Kutogunduwa (To be Overlooked) by Marc Eichen, translated by Shani Khalfan
1.
Unajua Binamu yangu Juma, ni rahisi sana kushughulikia vitu vidogovidogo na kushindwa kugundua vitu vikubwa; vile vitu ambavyo hatuvioni lakini vipo mbele ya macho yetu vinatuangalia.
Barabara inafungwa kwa hiyo wale wanaoitumia wanaweza kuipita bila hata kama wimbi. Lazima unafikiri daima ilikuwa hivi. Lakini nilipokuwa kijana, miaka mingi kabla hujazaliwa, ilikuwa barabara gani hii, mawe yaliyovunjwavunjwa? Na kabla ya hapo, ilikuwa udongo mwekundu, inaweka alama mvua zinaponyesha, muda mwingine tukipaliwa na vumbi katika baadhi ya majira ya mwaka?
Miaka mingi nyuma, baba yangu – alikuwa anakaa mbele ya duka letu, pale njia ilipomalizia akiuza matunda na mboga mboga. Wapita njia wangepunguza mwendo ili kumsalimia, kuulizia kuhusu familia yetu, kuhusu hali ya hewa, kuhusu Kidonge, kijiji chetu, na Shehia yetu. ilikuwa vigumu kwangu kuamini kuwa alikuwa akimjua kila aliyesimama lakini aliwakunjulia mikono wote. “Mnakaribishwa nyote kuungana nasi. Mungu amekuwa mwema hapa kwetu. Watoto watakuwa na afya. Mvua zitanyesha kwa wingi. Na mashamba ya majirani zetu yatatubariki kwa neema zao, vivuli vyao na matunda yao In sha Allah.”
“Naapa” sasa unaniambia, Juma,“Niliota haya katika ndoto zangu.”
Ninacheka. Kwa sababu unaposema hivi, unakunja uso kama kwamba umemkuta kupe ameganda sikioni mwako.
Je, maneno ya baba yangu yalikuwa dua? Labda alifikiri itakuwa kweli kama angesema mara mia moja au mara laki moja…kama angemwambia kwa kila mtu pale kisiwani, ingekuja kuwa kweli.
Tayari ulishakuja kuishi na sisi baada ya kufa wazazi wako na uliuliza pale msikitini, baada tu ya maziko ya baba yangu, “Nani wa kusema hizi dua hazikutusaidia, japo kidogo?
Lakini baba yangu alikuwa zaidi ya muuza duka mwenye bashasha; alikuwa Sheha wetu na msikilizaji mzuri. Kwa kila taarifa aliyoipata – mtoto wa kiume wa mtu yule ameowa na anaishi mjini nyuma ya msikiti wa Washirazi, mtoto wa kike wa mtu huyu, ambaye ni mkubwa kidogo kuliko wewe, alikufa mwaka jana kwa ugonjwa wa kisukari. – alipata mbili.
Baba yangu alikuwa akiniambia Mwenye Mungu amemjaalia subira ya kujibu swali kwa swali. Ulipofika muda wa kufanya mahesabu ya kodi na Ali, karani kutoka ZRB, aliuliza nyumba ngapi mpya zilijengwa katika Shehia mwaka uliopita, baba angesema “Rafiki yangu - nani anapaswa kusema nyumba ni nini? boma lile, lenye mzungu kichaa lililopo ufukweni ni nyumba? Je, vipi kibanda kile kilichopo ukishalipita shamba lile? Kuna familia inaishi pale sasa. Labda pengine wanakaa tu kama sisi sote mpaka Mungu awapeleke mahali pengine pazuri zaidi, kama sisi sote. Nyumba ngapi mpya zilijengwa? Hilo si swali rahisi. Hebu tupate chai na tulijadili.” Hata mimi niliweza kuona haya mazungumzo yangemalizika kwa kutuunga mkono.
Ndiyo, ndiyo. Ninajua. Mara kwa mara unanikumbusha, mimi pia ni mtu muhimu. Mimi ni Sheha wa Kidonge. Nafuata nyayo za baba yangu baada ya kufariki. Mungu ailaze roho yake mahali pema.
Nisingetaka kujigamba kupita kiasi, lakini nimeona mabadiliko mengi. Na kama ulivyoona wewe pia. Hukwenda hata skuli na hata kusoma au kusaini jina lako ni shida. Pia wewe umeishi na kuona barabara iliyofungwa, simu za mkononi na vyoo vya kisasa… Na sasa unacheka, Juma, kwa sababu hata wewe unacho kimoja. Alhamdulillah.
Unalalamika, Ndio, Huinui mikono yako juu. Ni kweli. Unauliza kwa nini lazima ununue maji kutoka kwenye magari katika siku ambazo maji yana ladha ya chumvichumvi. Unasema kuna kazi kidogo katika utengenezaji chandarua au kutengeneza baiskeli hapa na pale, kuleta chai ninapoomba na kusaidia jikoni. Ndio, ndio, Najua. Kuna kazi kidogo. Pengine ni kwa sababu tumebarikiwa na vijana wengi sana. Unasema baba yake hakutambui, hakusalimii unapomwona msikitini. Unaweza kumlaumu yeye, kwa ukweli? Anamtakia mazuri tu kwa mtoto wake wa kike. Na kipi unaweza kumpatia nje ya maisha ya mama yake na bibi yake?
Lakini maisha hapa sio mabaya. Kila asubuhi tunapoamka tunaona dunia ni changa na kijani. Tunajisemea wenyewe kwamba lazima ili tuishi kuona njia nyingi ambazo kwazo Mungu ametubariki.
Lakini kile tusichoweza kukiona . Kile tusichokiona…
“Ni nini hicho?” Unaniuliza “Ni nini tusichokiona?” Swali zuri, swali muhimu Nitakuambia.
Tusichokiona --- ni daraja.
Watu wanaotoka Kaskazini kwa daladala watamwambia dereva kuharakisha mpaka barabara inapoishia kwa ghafla mtoni, kama vile imekatwa kwa shoka lisilokuwa na makali, pembeni mwa mto. Na kisha mbali upande wa pili, ikiwa ukungu haujawa mwingi wanaweza kukitambua kijiji chetu. Wanaweza kuwaona watu wanarudi msikitini, wanawake wamezama nusu katika mashamba ya mpunga upande wa mashariki na watoto wakiruka nyuma ya mashuka na kanga zinazonin’ginia nje ya kila nyumba. Upepo unapokuja kutoka fukweni, wanaweza kusikia harufu ya moshi kutoka kwenye moto wa mkaa ambao inaokwa mkate. Ulipokuwa mtoto, Juma sio miaka mingi iliyopita, mto huo ulikuwa mwembamba. Unakumbuka? Nadhani ulikuwa na miaka saba ulipompiga Amina, alipofanikiwa akirusha jiwe upande wa pili wa mto. Alimwambia shangazi yake, aliyepiga kelele, ili kijiji chote kisikie, kwamba ujanadume wako ungekwisha usiku ule ule kama hujaomba msamaha. Unacheka, lakini unakumbuka mto ulipokuwa mwembamba kiasi mashua moja iliweza kuvuka kwa urahisi. Hata Issa, aliyeishi ukingoni mwa mto, na ambaye alikuwa mlemavu tangu farasi wake alipovunjika vidole vyake viwili, aliweza kubeba magunia kutoka upande mmoja na kuyapeleka upande wa mwingine.
Sasa mto huo kila mwaka unapanuka. Hakuna tofauti katika misimu. Wakati wa Ukame, hata, mtu lazima asindikizwe. Wageni wachache kutoka mjini iliwabidi waziache teksi zao na wavuke, huku wakijizuia kuanguka kwenye mawe. Na kama mtu anakwenda upande mwingine, kutoka kijiji chetu mambo ni yale yale. “Weka mguu wako hapa, lakini kuwa muangalifu katika sehemu inayobonyea kwenye ubao unaodidimia majini. Angalia. Usikanyage pale. Jiwe lile, ndiyo lile hasa litakuangusha.” Iwapo mtu anabeba kitu kizito, hawataweza kuvuka mto bila kijana kutoa maoni na msaada wake kwa kupewa bahshishi kidogo. Wanaitwaje wale? Aha, ndiyo, wanaitwa ‘wavushaji waongozaji?’
Mungu tunusuru wakati mtu mmoja anaanza kuvuka na mtu mwengine anakuja kutoka upande wa ufukweni. Unakumbuka wakati Idrissa alipokuwa akija kaskazini upande wetu huku akiwa na marobota ya vitambaa, na Momfrieda alikuwa akienda mjini upande wa kusini? Ninaweza kuona usoni mwako kwamba unakumbuka. Walikutana katikati, wakibishana kwa saa moja. Hakuna aliyekuwa tayari kumpisha mwenzake mpaka Momfrieda alipomtishia kumrushia Idrissa kila yai alilokuwa amechukua.
Na hayo yalitokea siku ambayo mbingu ilikuwa safi na hali ya hewa ilikuwa nzuri. Wakati wa mvua, mto unapokuwa unakwenda kwa kasi na mawe makubwa yanapokuwa yameondoshwa, hakuna hata mtu mmoja anayethubutu, hata yule mwenye nguvu kabisa katika wavushaji waongozaji hakuna anayethubutu kupita kwenye mto huo.
Watu wengine wa Kidonge huuliza — jambo hili lina umuhimu gani? Hakujawahu kuwa na daraja kamwe. Hivi ndivyo maisha yalivyokuwa tangu tulipokuwa watoto. Kwa nini sasa yabadilike?
Lakini huu ni mtanziko ambao baba yangu aliuelewa vyema. Kama ilivyokuwa hapo baadae, tuna Baraka kuwaona watoto wetu na watoto wao wakikua. Tunawaambia ndoto zetu na ndoto zetu zinakuwa zao. Haya ni maisha yetu na hatutayauza kirahisi. Hata hivyo, mto huu umepanuka na mvua za masika zinakuwa kubwa na za muda mrefu zaidi. Inapotokea hivyo, na vijana wanaogopa kuvuka, watoto hawawezi kwenda skuli na wazee hawawezi kwenda kliniki ya Masingini, au Mwera. Gesi ya propeni, sufuria za plastiki huzama matopeni katika ukingo wa ufukwe wakati tunasubiri. Daima huwa wa mwisho, kadri muda unavyopita kwa haraka zaidi, kuwa wa mwisho ni kuachwa nyuma milele.
Na ndiyo maana lazima niende mjini kesho asubuhi. Hii ni kwa nini, bila hata kikombe cha chai, nitakuwa nimesimama katika upande mwingine wa mto, kandambili zangu mkononi, miguu yangu ikiwa imerowa, tukiwa tunavuka mto wakati wa kiza.
Na wewe? Pengine ikiwa tunakwenda pamoja utaweka pembeni mawazo yoyote, wanasemaje kwa Kiingereza? Majani yatakuwa kijani zaidi mbali na barabara. Labda kama tunaweza kuleta daraja, wazee wa Kidonge watakufanya Sheha baada ya mimi kustaafu Au pengine, vyema, pengine napenda tu kuwa na wewe , kusafiri pamoja muda wote kuelekea mjini.
II.
Daladala, ambayo mwanzo ilikuwa pik’ap ya mizigo, ilitulia kama sehemu ya shamba. Ilikaa kama chura aliyepo katika shamba dogo mbele kidogo karibu na mti wa pekee, penye viti vibovu vichache, rundo la mabati ya kuezekea yaliyokaa ovyo na marobota ya taka taka za plastiki. Watoto wawili wa kiume walikuwa wakiuza peremende, sigara na kalamu katika hali isiyopendeza. Kwa namna walivyokuwa wakimwangalia kwa woga na wasiwasi, inawezekana waliajiriwa kazi ile na mtu, aliyevaa shati ya nailoni na Jaketi la Chelsea, akitumai kuuza chai kutoka kikombe kimoja.
Viti ndani ya gari vilivyokuwa karibu na dereva, kilichopinda magurudumu, anaforota, walipewa wanawake wazee walipoingia. Wengine waligoma kwa haraka kutoka gizani kujaza nafasi mbili za ovyo za mabenchi ya mbao yanayotizamana yaliyopo nyuma.
Wanawake wawili walikaa pamoja. Walikuwa wamevaa mabuibui meusi ambayo yaliyowafunika mwili mzima isipokuwa mikono yao, ambayo ilionesha mtindo wa hina, na macho yao, yalipambwa kwa wanja wa Omani. Vijana watano wa kiume wakinuka jasho na walikuwa wamevaa nguo zilizojaa dongo la zege, plasta na rangi walijipenyeza katika nafasi inayowatosha watu wawili tu. Mwanamke kijana mja mzito ambaye alionekana hazidi miaka 18 alipanda na mtoto wake wa kike, labda mwenye umri miaka 4 au 5 alipinda magoti chini ndani ya gari. Mzee mmoja mwanamme, mfanyakazi wa hoteli au wa serikali alikuwa amechukuwa jalada lililochanika na alikaa katika benchi upande wa Juma.
Wakati daladala ilikuwa imekaribia kujaa, konda alirukia kibao cha gari kilichopo nyuma ya gari na kwa kutumia pesa aligonga mara mbili kwenye fremu za paa la gari. Dereva aliamka na wakati huohuo aliachia breki na akawasha gari huku meno ya gia iliyovunjika yakianguka chini pamoja.
Kila masafa ya mita mia mbili au mia tatu, dereva alivuta ovyo ovyo au kuchukua – au kupita, bila kuomba msamaha au kutoa maelezo – abiria zaidi. Konda aligonga kwenye fremu mara moja ya gari ili abiria kuweza kushuka na baadae alingonga mara mbili au kupigaga kelele “Tembea” ili safari iendelee. Mabenchi yote yalipokaliwa, lakini bado kulikuwa na nafasi ya kupinda magoti au wanaume kwa pamoja kuning’inia nyuma ya gari.
“Unaenda mpaka mjini?” aliuliza yule mtu mwenye jalada lililochanika.
“Ndiyo” Juma alijibu huku Abubaker akimbonyeza kwa kiwiko mbavuni.
“Huhitaji kumwambia kila mtu”.
“Sikusudii kudadisi,” yule mtu aliendelea, “lakini sielewi namna ulivovaa. Hili lazima liwe tukio muhimu.”
“Ninakutana na Waziri wa Huduma za Umma,” alijibu Abubaker. Na kisha akamwambia
Juma kimya kimya, “Hataniamini kama nitamwambia sote wawili tunakutana na Waziri.”
“Hongera. Lazima wewe ni mtu maarufu.”
“Katika Kidonge.”
“Ah ndiyo. Mahali padogo tu upande wa pili wa mto. Sijawahi kufika kule, kwa sababu unajuwa, hakuna cha kufanya .”
“Ni mahali penye amani.”
“Upuuzi.” Yule mtu alicheka. “Ni kama mamia ya vijiji vingine vyovyote tutakavyovipita tunapokwenda mjini asubuhi hii.”
Abubaker kwa huzuni kubwa mbele ya Juma, hakuweza kupata jibu, kufikiria kitu chochote kinachoweza kupafanya Kidonge kuwa mahali stahiki pa kutembelewa, na mahali mashuhuri sana.
“Umewahi kufika mjini kabla?”
“Juma hajawahi. Lakini yupo pamoja nami. Anafikiria kuishi mjini. Unaweza kufikiria hivyo?” Abubaker alichekelea, akitafuta kuungwa mkono kwa mawazo haya ya matarajio yasiyowezekana.
“Niruhusu,” yule mtu allisema, huku akinyanyua nyusi zake kwa mshangao, “nikwambie kitu, siku hizi laziama uwe mwangalifu mjini. Angalia pesa zako hasa unapokuwa sokoni. Kuna vijana wa kiume pengine wageni kutoka Kongo au Nairobi wanaohusika na madawa ya kulevya” Wanawake wote kwa ghafla walionekana wakisikiliza kwa makini. Walitikisa vichwa vyao wakionesha kukubaliana.
Juma alimsikiliza wakati Abubaker akimjibu.
“Kwa hiyo unaniambia kuwa sasa mjini ni mahali pa hatari?”
“Ndiyo, ni kweli.”
“Na nimesikia ni mahali ghali”
“Ni gharama kupata sehemu ya kuishi” Yule mzee alipasha maelezo yake mwenyewe juu ya maisha ya mjini, “Na hakuna ardhi ya kuotesha chakula chako mwenyewe”
Wakati Abubaker akitikisa kichwa chake kujaribu kujenga picha ya mahali wanapokwenda, Juma aliyaangalia mashamba ya kijiji huku wanayapita. Mfanano wake na Kidonge ulimfanya kushangaa jinsi maisha yake wanavyoweza kuwa tofauti, tofauti na kina Juma wengine katika kila kijiji cha kisiwani
Isipokuwa kwa wafanyakazi, ambao walikuwa wamelala mara tu walipoingia na waliegemeana kama marundo ya nguo chafu, kila aliyepanda daladala alionekana kumjua mtu mjini na alikuwa anapanga kukaa huko angalau kwa siku chache.
Mmoja wa wanawake waliovaa buibui, “Nina binamu anayeishi Amani na mwengine Mwanakwerekwe.”
“Nitakwenda kukaa kwa dada yangu kwa siku chache huko Kiembe Samaki,” aliongeza mwengine.
“Tembea.” Konda aliruka nyuma ya gari na daladala ilirudi barabarani.
“Oh ndiyo, ” Juma alisema bila kumwambia mtu maalum, Amina anaye kaka na Yasir Ali, mjomba wake anamiliki boti.”
“Inaelekea siku hizi mjini panaweza kuwa mahali pabaya sana.” Uso wa Abubaker ulionekana kama aliyekula samaki aliyeoza. “Kwa nini mtu ungependa kuishi hapa?”
Yule mwanamme mzee aliinamia mbele wakati daladala ilipopinda ghafla ili kukwepa, “Ninaweza kukusimulia hadithi?”
“Bila shaka. Wakati utapita kwa haraka zaidi.”
“Binamu yangu alikuwa na kikataa kidogo sana kusini mwa kisiwa ambako familia ya mke wake walikuwa wakiishi. Jirani yake alikuwa na watoto wanne, mtoto mmoja wa kike na watoto watatu wa kiume.”
Yule mwanamme mzee alimpa lile jalada kwa mwamammke mmojawapo ili yeye aweze kuashiria kwa mikono yote miwili huku akiendelea.
“Mtoto wa kiume mkubwa alikuwa mtundu sana. Alipiga fundo nyavu ya mtu huyu au kumrushia mawe ngo’mbe wa mtu yule. Dada yake mkubwa, ambaye alikuwa na kazi ya kuwatunza watoto wadogo, alikuwa akimpiga na kisha jioni alipofika nyumbani baba yake alikuwa akimpiga tena. Walimwita dafu kwa sababu alikuwa sugu kwa kipigo. Huwa mzuri kwa siku chache, akienda skuli, akitumwa huku na kule na wazee wa kjijini. Na baadae wiki inayofuata ataanza utundu wake tena.”
“Mwishowe babayake alimwambia angepata kazi aidha katika boti ya kuvulia au wangempeleka mjini aishi na mjomba wa binamu yake.
“Bila ya kufikiria zaidi, alichagua kwenda mjini. Familia yake walimpandisha daladala, na walimwambia mjomba wake alikuwa na genge sokoni na angeweza kumuuliza mtu yeyote ili aweze kuliona. Walimwambia awatumie pesa atakapoweza.”
“Mjomba wake alimpa kazi ya kutumika hapa na pale na kuliendesha genge wakati alipokuwa msikitini.” Ndani ya kipindi cha mwezi mmoja alipata simu iliyotumika na aliweza kumtumia pesa mama yake. Na katika muda wa chini ya mwaka mmoja aliweza kukopa pesa na kufungua genge lake mwenyewe sokoni. Katika miaka michache alikuwa na mke, nyumba na watoto mapacha.”
“Nyumba na … mke? Na baada ya miaka michache tu. Allah kareem.” Juma alijisemea huku akifikiria fursa zake ndogo pia.
Abubaker aliangalia chini ya daladala. Pole pole kwa sauti ya chini alisema, “Nimesikia kuwa watoto mapacha ni bahati mbaya.”
“Ninajua hadithi ya kushangaza zaidi, alisema mmoja wa waashi ghafla akitoka usingizini. “Rafiki yangu anamjua kijana wa kiume ambaye alifanyakazi katika hoteli huko mjini. Alikwenda chumbani kutengeneza taa na mwanamke wa kizungu aliyekuwa akikaa kule alimuomba amsaidie kubeba mabegi yake kutoka sokoni. Chini ya wiki mbili baadae, walioana Alipata ujauzito na alifanya mipango ya wao kuishi nje ya nchi, katika Ulaya.”
“Mmoja wa wanawake aliyevaa baibui alitikisa kichwa “Unaweza kutarajia nini kutoka kwa mwanamke? Mwanamme atarudi ndani ya mwaka mmoja. Wanajua nini kuhusu kuolewa?” “Usiamini kila unachosikia,” Abu alimwambia Juma.
“Ndiyo “ Juma alijibu, “lakini lazima kuwe na ukweli katika hadithi hizi. Kila mtu inaonekana ana hadithi.”
“Sote tumesikia hadithi kama hizo,” alisema mzee wa kiume. “Na nani anajua kama kila kitu ni kweli katika maelezo. Mjini ni mahali watu wema na waovu wanapoonekana. Utayaona yote hayo. Lakini sio unachokiona ndio muhimu. Ni kile ambacho hukioni.”
“Kipi usichokiona…” kila mtu katika daladala alisogea mbele kuhakikisha anasikia.
“Usichokiona ni kwamba mji unafanya mambo yawezekane.”
Wakati mtu akiegemea na kukunja mikono yake akiashiria kwamba ilikuwa mwisho wa hadithi, kila mtu katika daladala alianza kutoa maoni yao kuhusu jambo hili. Mtu mmoja alisema jambo hili linawezekana ni njozi. Allah ameamua litakalokutokea kutokea siku uliyozaliwa. Uwezekano mwengine uliotajwa ulikuwepo tu kwako ikiwa familia yako ina pesa. Na wengine wanasema mafanikio kama hayo yalikuwa yanawezekana ikiwa tu unauza madawa ya kulevya au unafanya uhalifu.
Wakiwa abiria wanajadiliana na Abubaker akisinzia, Juma aliangalia njia zilizokufa za vijiji vinavyopita na huku akirudia kimya kimya peke yake “Mji unafanya mambo yawezekane, mji unafanya mambo yawezekane.” kwanza kwa mshangao lakini halafu, kama vile anajadiliana na mwishowe katika makubaliano. Lakini jambo asilokuwa na hakika nalo.
Katika chumba cha wanaosubiri cha Wizara, Abubaker alikosha mikono yake na Juma kwa umakini alirekebisha kanzu yake, akinyoosha ukosi na akivuta mikono, ili kuhakikisha kuwa zinamfanya kuwa na ushawizhi mzuri. Baada ya saa ya miadi walikaribishwa katika ofisi ya Waziri, Abubaker akiongoza na Juma akifuata kwa karibu nyuma. Ingawa Abubaker alitaka kufanya ionekane kama alikwenda mahali pale kila siku, wote walipigwa na mshangao wakati mlango kuelekea ofisini ulifunguliwa. Kulikuwa na kiyoyozi na mafeni kadhaa yakizunguka juu ya vichwa vyao. Mchanganyiko wa jasho na vumbi la safari liliganda nyusoni mwao na chini ya nguo zao.
“Juma, joto hili. Hali hii lazima ilete hisia ya kuishi hasa ni nini,” Abu alisita, “Ulaya.”
Pamoja na hili, Wote wawili walishangaa kumuona mwanamke amekaa nyuma ya meza ya Waziri. Kwa muda wote walidhani kuwa wamemkamata mmoja wa wasaidizi wa ofisi akisoma nyaraka rasmi. Lakini alipozungumza, waligundua kuwa alikuwa hasa Waziri wa Huduma za Umma.
“Ah, Babahamid, Mzee, Shikamoo. Karibuni kaeni.” Alionesha, na walikaa juu ya viti viwili vidogo, vigumu. Ukubwa wa meza ya mbao na rundo la nyaraka zilizokuwepo juu yake ilifanya ielekee kuwa kichwa chake kilikuwa kikiruka kama meli iliyokuwa juu ya mawimbi ya karatasi.
“Marahaba, bibi,” alijibu Abubaker.
“Niambie mambo yalivyo katika …” Waziri aliangalia karatasi iliyokuwa mbele yake,“Kidonge?”
“Maisha ni mazuri. Watoto wanakua na wazee wanaheshimiwa.”
“Ah, maisha nchini. Yako safi. Ninaamini safari yenu haikuwa na matukio?”
“ Haikuwa na matukio, ashukuriwe Mungu. Ndio sote hatujambo Na familia yako?”
“Mambo yanaendelea vizuri. Naamini baba yako alikuwa anamjua baba yangu, Sheha wa Vuga.”
“Ah ndiyo.” Uso wa Abu ulisisimka kwa mfadhaiko wa ujinga. “Baba yangu alimzungumzia mara kwa mara. Alikuwa mwanazuoni.”
“Alichochea mapenzi ya kusoma kwa watoto wengi. Mimi nilikwenda Chuo Kikuu cha Kampala.”
“Mafanikio mazuri sana.”
Walikaa kimya kwa muda mfupi. Juma alikuwa anajua kuwa kuna saa isiyooneka inagonga sehemu fulani ofisini.
“Ninaweza kukusaidia nini asubuhi hii njema?”
“Unakijua kijiji chetu? Kiko barabara ya kwendea kaskazini, bila shaka.”
“Bila ya shaka.” Waziri aliziangalia tena karatasi zilizokuwa mbele yake. “Kidonge. Ninakijua. ni mahali pazuri.”
“Ni kizuri na tunakitunza. Mungu anatoa na tuna mahitaji machache.
“Kwa hakika, Mungu anatoa. Ukilinganisha na Mungu, Wizara ya Huduma za Umma inaweza kutarajia kutoa nini?”
“Kweli, lakini vitu vingine vidogo vidogo vimo zaidi katika uangalizi wa Wizara kuliko kuwa katika uangalizi wa Mungu. Nilikuwa natumaini, tunatumanii, kupata msaada wako—.”
“Bila ya shaka,” Waziri alitikisa kichwa, “nipo hapa kwa ajili hiyo. Tupo sote hapa kwa ajili ya gani”
“Unaona, barabara ya kwendea kaskazini ni —”
“Iko vizuri. Ingawaje siendi Kidonge mara kwa mara kwa vile ni mbali kule, ninaendesha mara kwa mara, kwenda na kurudi katika gari la waziri. Ili kuthibitisha hali hiyo.”
“Kwa hakika, wafanyakazi wa Wizara wanakuja mara kadhaa kuitengeneza barabara hiyo kila mwaka. Barabara inakwenda mpaka inafika mtoni, na hilo ndilo tatizo.”
“Hapo pana tatizo gani?”
“Sawa Bibi Waziri, niseme nini. Barabara inakwenda mpaka mtoni lakini haivuki mto.”
“Barabara karibu zote hufanya hivi, huishia hatimaye.” Waziri alicheka kwa mzaha wake mweyewe.
“Ndiyo, ndiyoMheshimiwa.” Abu pia alicheka kwa haraka. “Lakini kungekuwa ufanisi… zaidi kama kungekuwa na … daraja.”
“Daraja?” Waziri aliziangalia karatasi zilizokuwa juu ya meza kama vile Ukweli ulikuwa umo mle na kama angeweza kuupata.
“Ah ndiyo ipo hapa. Kumekuwa na ombi la daraja kwa miaka mingi. Lililofanywa na” alipekuwa tabaka kadhaa la karatasi, “baba yako mzazi”. Baba yako. Lazima wakati huo ulikuwa kijana alipofanya maombi hayo,.”
“Ni kweli, Mheshimiwa.”
“Ninaweza kuona kuwa Chama na Serikali, baada ya miaka mingi, wamelikubali ombi hili hivi karibuni, na kwa uungaji wangu mkono wa nguvu zote. Na sio daraja tu — daraja la kisasa, lililojengwa kwa kangriti na vyuma.”
“Na sisi tunashukuru sana Mheshimiwa. Bila ya msaada wako mkubwa, sis ni kama… hata maneno yananishinda.”
Katika muda huu, Juma alizungumza, akiwashtua Waziri na Abubaker, “Ndiyo Bibi Waziri sisi watu wa Kidonge ni kama mbatata ndogo tu. Na bila ya msaada wako, Bibi Waziri, tutaendelea kuwa mbatata mbichi. Hilo ndilo tatizo.”
“Mbatata mbichi. Hilo ni tatizo kubwa. Lakini samahani, huyu ni nani?”
“Tusamehe bibiye mtukufu, huyu ni msaidizi wangu …Juma.”
Waziri alimuangalia mtu mmoja mmoja, “Karibu, Msaidizi Juma.” Aliendelea, “Kwa hiyo ikiwa daraja, daraja la kisasa limeshathibitishwa kujengwa tayari, tatizo ni nini??”
“Tatizo,” Abu alisema polepole, “ni kuwa mto umekua. Kutokana na wakati, umepanuka.”
“Mto ni mpana zaidi sasa. Waziri aliziangalia tena karatasi. “Na kama daraja ni la kisasa kwa nini hilo ni tatizo?”
Kwa kujiamini Juma alizungumza tena “Umethibitisha nusu daraja.”
“Jambo hilo linawezekanaje? Ni kweli kwamba Chuo Kikuu nilisomea zaidi Sayansi ya Maktaba na siyo Uhandisi. Lakini ningewezaje kuthibitisha daraja linalokwenda upande mmoja tu?”
“Hapana, hapana, Mheshimiwa,” alisema Abu, “si hivyo kwamba —”
Kwa mshanagao wa Abu, Juma alimkatiza tena.
“Mto umekua. Umekuwa mpana zaidi. Daraja la kisasa ulilolithibitisha litakwenda nusu tu ya kuvuuka mto.”
Pamoja na kumkatiza kwake, Waziri aliepuka kumuangalia Juma wakati akizungumza, “Sawa kwa hiyo.” “ndiyo hivyo.”
“Kuna nini, Mheshimiwa?”
“Ndiyo hivyo,” alirudia. “Si kosa letu. Angalia karatasi hii, ipo wazi. Sisi tumethibitisha ombi la baba yako pamoja na miaka mingi kupita. Na hiyo ndiyo makisio yetu yote ya matumizi.”
“Ndiyo, Mheshimiwa, lakini —”
“Baba yako angetaka daraja refu zaidi, angeiomba, ”
“Lakini, Mheshimiwa —”
Waziri alizichanganya zile karatasi, alilifunga jalada lililokuwa juu ya meza yake na alisimama kutoka kwenye kiti chake, “Kwa kweIi nimefurahi kuwa na mkutano huu. Mnajua Serikali, na bila shaka Chama, siku zote kina furaha kusikia kutoka kwa masheha wengi kama inavyowezekana. Japo wale kutoka maeneo madogo na mashambani. Inatukutanisha na watu tunaowahudumu”
Mkutano ulimalizika. Abu na Juma walisimama ili wasimuudhi Waziri. Lakini alifungua wakati anafungua mlango, Juma alimnon’goneza Abu sikioni, “Hajui kuhusu daraja. Anajua kuhusu … makisio ya matumizi. Muombe msingi tu, msingi unaozuia daraja.”
“Mheshimwa, ninaweza kupata dakika moja ya muda wako wa thamani?”
Waziri alitazama saa yake. “Tuna kazi nyingi hapa, lakini sawa.”
“Unaonaje ikiwa badala ya nusu daraja,” Abu alianza, “serikali ingejenga msingi wa kangriti na chuma? Na sisi, raia wa Kidonge tungeongezea barabara ya mbao.”
“Mnataka Serikali ijenge msingi tu?”
Akiwa amesisma nyuma ya bega la Abu, Juma alijibu, “Ndiyo. Msingi ungeweza kuvuka mto mpana. Wavushaji waongozaji wetu na wanaume wa kjijini wangeweza kuongeza vifaa vingine vya mbao vya barabara kama mto ukiongezeka siku za mbele.” Alisita na Juma aliutumia muda huo.
“Tutajenga njia ya barabara kwa gharama zetu wenyewe. Wizara haitagharamika sana.”
Waziri alionekana kulizingatia jambo kwa muda na akatikisa kichwa kwa kukubaliana nalo, “Abubaker, hiyo ni fikra nzuri sana. Nina furaha kwamba jambo hili tulilizingatia pamoja. Ni ufumbuzi wa ubunifu kwa tatizo sugu. Wacha nimuite mmoja wa wahandisi wangu.” Alipiga namba fulani kwenye simu yake na akaongea kwa dakika chache.
“Anasema, timu yake itajenga vizuizi vya daraja mtoni kwa kangriti na vitakapokuwa vimetulia, wanaume kutoka Shehia yako wanaweza kujenga tandiko la barabara kwa mbao. Timu yetu ya ujenzi wa barabara wataendelea kuindeleza siku za mbele. Ikiwa jambo hili limekubaliwa, alisimama na watatu hao walisogea mbele huku walikuwa wanaangalia kupitia dirishani mustakabali wao, baadae nitawaandikia barua fupi kwa wa Idara ya Uhandisi. Suala hili limekwisha.”
III.
Joto la mchana lilikuwa limeanza kupungua kukaribia jioni wakati tunaondoka ofisi ya Waziri na tulitembea kuelekea sokoni. Kanzu zetu zilikuwa zimebadilika kidogo na vumbi ka siku hiyo, lakini hakuna aliyeonekana kugundua. Mwenyeduka alimita Abu, akimtaka anunue madebe ya plastiki, dawa za meno, vifaa vya jikoni, visu vikali, ambavyo vyote havipatikani shamba. Katika vumbi linalozunguka na kelele, hatukutendewa tofauti na watu wengine — wageni, Malaya, wafanya biashara na maimamu — lakini pengine hatukutendewa vibaya zaidi. Abu alinunua viungo kutoka Pemba, pamoja na korosho na matofaa kutoka bara aliyoagizwa na mpishi wake. Nilinunua kanga maalum katika maduka ya juu yaliyoko upande wa pili wa barabara na Abu hakutaka kujua ni kwa ajili ya nani wakati aliponipa pesa kununu maandazi na chai. Tulikaa pamoja na kupumzika katika meza ndogo nyuma ya kituo cha petroli cha Gapco.
“Nadhani, Juma ninapaswa kukushukuru.”
“Kwa jambo gani?”
“Vizuri, Unajua.” Abu alirekebisha vifurushi na akanywa funda la chai “Kwa suluhisho lako la tatizo letu . Una akili nzuri ya biashara. Mambo haya yatakwendea vizuri itakapofika wakati wa kuzingatia Sheha anayekuja. Ndiyo lazima nikushukuru kwa —”
“Unajua baba, mimi ni kiungo kidogo tu katika mnyororo.”
“Una maana gani?”
“Kama usingenialika katika mkutano huu, kama msaidizi wako, ingekuwa nini? Na kabla ya hapo, kama Kidonge wasingekuomba kukutana na Waziri, tungekuwa wapi? Na hata kabla ya hapo, miaka mingi iliyopita, ingekuwa baba yako hakufanya ombi lake la mwanzo ingekuwa nini?”
“Na unadhani kila hatua katika hili ilikuwa muhimu?”
“Nafikiri kila moja --- wanasemaje kwa Kiingereza? muhimu, , muhimu lakini umoja tu unatosha.”
Kila mmoja wetu alikunywa mafunda na chai na kipande cha andazi.
“Na unajua, Abu, nadhani tusipofanya haraka, itakubidi usimame katika dalalada mpaka mtoni kwetu kwa daladala.”
“Mimi,” nilisema. Nikinywa funda la chai na nikasikia kelele za sokoni mbele yetu. “Nafikiri sitarudi Kidonge, japo kwa leo tu. Nadhani nitakaa hapa mjini na nitajaribu kufanya vitu fulani.”
Ilikuwa kama nimempiga Abu kwa jabali.
“Unatania?”
“Hapana kabisa. Unakumbuka uliponiambia ilikuwa muhimu kuona kisichoonekana? Unakumbuka hadithi ya kijana wa kiume alituhadithia kwenye daladala. Ninataka kujaribu kutafuta maisha yangu yatakuaje, kipi nisichokiona bado. Kufanya hivyo, ninahitaji kuishi hapa. Labda ninaweza kumshawishi Amina aje na adai kanga nilizomnunulia. Labda ninaweza kumshawishi baba yake kwamba mimi ni zaidi ya punguani, nisiyekuwa na thamani hata ya kusalimiwa. Au labda sivyo.”
“Lakini vipi kuhusu Sheha ajaye? Vipi kuhusu mustakabali wako… katika Kidonge? Ndiyo, sasa huna elimu. Unafanya kazi mashambani. Sasa wewe ni,” Abu alipata kigugumizi, ikaonekana kama anataka huku hataki kusema wazo lake, “hamna kitu.”
“Hasa. Na hiyo ndio maana nataka kuishi na kujaribu bahati yangu hapa. Hata kama nitakuwa Sheha, itakuwa miaka mingi ijayo, mimi sina elimu. Sina ardhi, wala utajiri. Kwa walio wengi katika Kidonge, siku zote nitaonekana si chochote. Maisha yangu yatakuwa kama daraja ile isioyokwenda popote.”
“Sijakusudia hivyo.”
“Ndivyo ulivyokusudia. Na umesema ukweli, Baba. Kwa hiyo tafadhali niache nimalize.”
“katika Kidonge, hayo ndiyo maisha yangu sasa, na ndivyo maisha yangu yatakavyokuwa kwa muda wa maisha nitakayoishi. Lakini nikija hapa, mjini maisha yangu yanaweza kuwa vingine.”
“Kwa hiyo unataka kuwa mmoja wa wale?…” Abu aliwaonesha watu wanaojaribu kukokota mikokoteni ya mbogamboga iliyovunjika maringi.”
“Ni kweli baba hapa ndipo maisha yanaanzia kwangu. Ninaweza kuwa ringi lililovunjika, mwanzoni. Lakini ukijitahidi vya kutosha hata maringi yale yanaweza kuzungukal. Hakuna uhakika Mwalimu mdogo amenifundisha Kiingreza kidogo na umesema mwenyewe. Nina akili ya biashara. Kama Mungu ni mwema kwangu, na nikipata bahati, hapa nina fursa ya maisha tofauti, maisha ambayo hayajaandikwa toka nilipozaliwa. Kwa sababu hii, nitakaa mjini.”
Abu alikichukua kikombe changu na akapangusa vumbi kanzu yangu. Tulitazamana.
Macho yake ya kahawia yalikuwa na maji maji na ngozi yake iliakisi jua lianalotua bandarini. Kwa juu ya bega lake niliona kivuko kikitoka bara na mashua za wavuvi zikiruhusu upepo uwachukue kwa kazi ya usiku.
“Nitakwenda msikitini kesho asubuhi na kukuombea dua,” alisema. “Zaidi kukuombea kwa mustakabali wako wa baadae.”
“Namwomba Allah azikubali dua zako.”
Tulitakiana safari njema. Kwangu mimi popote Mungu atakaponipeleka. Na kwa yeye kurudi Kidonge. Mahali ambapo watoto wanashirikisha ndoto zao na Sheha anajibu swali kwa swali. Mahali pembeni tu ya barabara inaishia, ambapo mto hukutana na bahari.